Katika
kipindi hiki cha kukaa ndani watu wamepunguza mizunguko ambayo inasaidia kama
mazoezi madogo madogo. Sasa leo naomba tujifunze ni namna gani mtu anapata
kitambi, Kitambi ni nini hasa? Nitatumia njia ya input na output (kinachoingia
na kinachotoka)
Nimechagua
mfumo wa input na output maana hiki ndio kinachotokea hata kwenye mwili mpaka
mtu anapata kitambi. Input nikiwa na maana "kinachoingia" na output
''kinachotoka". Nikwambie tu hicho kitambi ni store ya mwili ya kutunzia
chakula.
Mwili
unahitaji nishati (energy) ili kufanya kazi, Nishat kubwa ya mwili ni sukari
(glucose) tofauti na sukari tunayokunywa kwenye chai, Chanzo kikuu cha sukari
hii ya mwili ni wanga (carbohydrate). Je inakuaje mpaka wanga unakua sukari?
Unapokula
chakula hiki kinapofika tumboni mwili hukichanganya na kukilainisha chakula kwa
kutumia kemikali na enzymes. Sasa niseme tu mwilini chakula kinapoingia kuna
askari kazi yao ni kusubiri chakula kilainishwe kisha wakichukue kukipeleka
sehemu husika. (askari ni mfano).
Kama
ilivyo huku uraiani, kila askari ana kikosi chake na kazi yake maalumu. Kuna
atakaebeba protein, kuna wa wanga, kuna wa vitamin n.k. Kila askari na aina ya
chakula chake.
Leo acha tuongelee wanga ambayo ndio aina ya chakula
inayotufanya tujadili mada hii ya kitambi.
Sasa
baada ya wanga (carbohydrate) kulainishwa hubadilika na kuwa glucose ambayo
ndio sukari ya mwili. Basi askari ataibeba ile glucose tayari kuipeleka kwa
ajili ya matumizi mwilini. Askari huyu ataipeleka kwenye mfumo wa damu ili
isafirishwe sehemu zote za mwili.
Sasa
akifika katika lango kuu la mfumo wa damu anakutana na askari wengine wanaitwa
Insulin. Askari hawa kazi yao kubwa ni kuhakikisha kiasi cha sukari kilichopo
kwenye damu hakizidi kiwango kinachohitajika ndio maana kutokuwepo au utendaji
mbovu wa isulin husababisha kisukari.
Insulin
atakapoipokea sukari hii kabla ya kuruhusu iingizwe kwenye damu au la
anaangalia kama kwenye damu kuna kiwango cha sukari kinachofaa. Kama hakitoshi,
inaruhusu kuingizwa, Lakini kama kinatosha inazuia sukari zaidi kuingia na
kuamuru sukari hiyo ipelekwe kwenye stoo.
Stoo
za mwili ni ini na misuli (liver and muscles).
Baada ya insulini kusema sukari
inatosha, Sasa ili sukari hii ihifadhiwe kwa matumizi ya baadae inabidi iwe
katika mfumo utakaodumu kwa muda mpaka mwili utakapoitaji sukari ya ziada.
Mfumo huu unaitwa glycogen.
Glycogen
inahifadhiwa kwenye ini, mwili ukihitaji sukari na tumboni kukiwa hamna kitu
basi hutuma askari kwenye stoo hii na kuchukua gkycogen kisha kuibadilisha kuwa
glucose na kisha kuingiza kwenye mfumo wa damu.
Glycogen ndio sababu hatuli
kila baada ya dakika kadhaa. Sasa
ukila kwa wingi carbohydrate (wanga) kiasi cha kufanya stoo ya mwili (ini)
kushinwa kuhifadhi wanga huo na kwasababu mwilini wanga unatambulika kuwa
muhimu mwili hauwezi kutupa bali hubadilisha kuwa mafuta (fats or adipose
tissue) ambayo itatuzwa kwa muda mrefu.
Hizi
fats na adipose tissue hupelekwa na kutunzwa kwenye tumbo, hips, mapaja na
makalio. Hivyo basi utumiaji wako wa sukari ya mwili ndio utasababisha mwili
aidha uendelee kutunza mafuta au uyabadilishe na kuyatumia. Hapa ndio tunafikia
hatua ya input na output.
Input
inabidi iwe sawa na output. Unachoingiza mwilini inabidi kiwe sawa na
unachotumia, Kama mwili haujishughulishi inabidi uzingatie nini unakula,
ukiendelea kula wanga kwa wingi huku huzingatii matumizi yake unalimbikiza
mafuta mwilini.
Kazi kubwa ya wanga ni kuupa mwili nguvu
Unaposikia
njaa haimaanishi mwili unahitaji chakula la hasha bali ni kwa sababu umeuzoesha
mwili, ukiuzoesha mwili muda muda flani ukifika unaweka kitu tumboni basi kila
muda ukifika mwili unajiandaa kupokea chakula, askari wanakua tayari
kusafilisha chakula, kemikali zinamwagwa.
Utashangaa
ukiacha kula muda mrefu njaa itauma lakini itafikia wakati itaacha mwili ukiona
hamna chakula na kama una uhitaji wa chakula safari kwenye stoo na kuchukua
chakula kilichotuzwa. Ndio maana mtu mwembamba na mnene wakikaa muda mrefu bila
kula mwembamba atadumu muda mfupi.
Ushauri
wangu, kula endapo tu unasikia njaa, usile kwa sababu muda wa kula umefika.
Ahsante sana kama umesoma mpaka hapa, Mungu akubariki.
0 Comments