Leo nitaongelea juu ya
uhakika wa vipimo vya maabara kwa kuzingatia vitu viwili ambavyo huzingatiwa
wakati wa utengenezaji wa vifaa vya kupima magonjwa maabara, Vitu hivi ni Sensitivity vs Specificity.
Vipimo vya maabara huwa
sahihi kama ukipima kile kinachotakiwa kupimwa. Njia ya upimaji tutasema ni
bora pale ambapo kipimo kimoja kitapimwa zaidi ya mara moja na kutupa majibu
yanayofanana. Kwa kifupi hapa tunamaanisha usahihi wa kipimo.
1. Sensitivity.
Ni ule uwezo wa kipimo
kugundua watu walio na ugonjwa. Mfano: Kipimo kimehakikiwa kuwa 90% sensitive.
Hii inamaanisha, Kama watu 100 wanaojulikana kuwa na ugonjwa wakipimwa, watu 90
kati ya 100 watakutwa na ugonjwa.
Unapoongelea
sensitivity ya kipimo unaongelea ule uwezo wake wa kusema huyu mtu ana ugonjwa
ikiwa kweli anao (test positive when disease present). Kipimo chenye uwezo huu
kikikupa majibu negative basi ni hakika hamna ugonjwa kwa mtu husika.
Kwa lugha nyingine
naweza sema vipimo vilivyotengenezwa kwa uwezo mkubwa wa sensitivity haviwezi
kukosea iwapo kuna ugonjwa kwa mtu husika hivyo kuwa na uhakika kama majibu
yakiwa negative. Majibu ya kipimo kilicho na uwezo mkubwa wa sensitivity huwa
ya kuaminika yakiwa negative.
Kwanini nasema majibu
negative huaminika? Kipimo hiki hakiwezi kukosa ugonjwa kama ugonjwa huo upo,
ubaya wa kipimo hiki ni kuwa hata ikitokea kuna ugonjwa mwingine unaoendana na
ugonjwa unaopimwa bado itasema positive ndio maana kikisema mtu hana ugonjwa ni
kweli hana.
Najua nimekuacha kidogo,
Upande wa wadudu waambukizao magonjwa kila mdudu ana familia yake. mfano huyu
coronavirus ana familia kama MERS na SARS, sasa kipimo cha sensitivity kubwa
kitapima uwepo wa kirusi cha corona bila kujali ni SARS au MERS maana ni
sensitive kwa coronavirus.
Sasa ukitaka kutafuta
wagonjwa wa MERS-Cov huwezi kutumia kipimo cha sensitivity maana kitakupa
majibu hata ya SARS-Cov. Ndio maana nimesema majibu ya negative kwa kipimo cha
sensitivity kwa asilimia kubwa huwa yenye uhakika na ni kweli mtu huyo hana
ugonjwa. Natumai umeelewa mpaka hapo.
2. Specificity.
Huu ni ule uwezo wa
kipimo kugundua watu wasio na ugonjwa. Mfano: Kipimo kimehakikiwa kuwa 90%
specificity. Hii inamaanisha, Kama watu 100 wasio na ugonjwa wakipimwa, watu 90
kati ya 100 watakutwa hawana ugonjwa.
Specificity ya kipimo
ni ule uwezo wa kusema huyu mtu hana ugonjwa ikiwa kweli mtu huyo hana ugonjwa.
sasa tukirudi kwenye mfano wangu hapo nyuma wa SARS na MERS. Kipimo
kilichotengenezwa kuwa na uwezo mkubwa wa specificity huwa maalumu zaidi kwa kile
unachopima.
Mara nyingi vipimo hivi
hutengenezwa maalumu kwa ajili ya mdudu fulani maabara huwa tunaita ni
confirmatory test. Mgonjwa atafika utampima na kipimo cha sensitivity ikiwa
negative utaishia hapo na kutoa majibu, ikiwa positive utaendelea mbele na
specificity kujua ni mdudu gani.
Vipimo (sensitive na
specific) huwa tofauti hata kwa gharama na upatikanaji wake. Kilicho na uwezo
mkubwa wa specificity huwa ngumu kupatikana na gharama yake huwa juu maana huwa
maalumu zaidi kwa ugonjwa/mdudu. Ni muhimu kutumia vipimo vyote kabla ya kutoa
majibu ya positive.
Niwape stori kidogo,
Wakati nipo chuo iliwahi kutokea kesi moja. Mdada mmoja alitaka kwenda kupima
ukimwi lakini kutokana na aibu ilibidi aongee na jamaa yake ambae ni nesi pale
hospitali amchukulie kipimo cha ukimwi (bioline) ili apime akiwa nyumbani na
jamaa alifanya hivyo.
Sasa kama nilivyosema
kuna vipimo vyenye uwezo mkubwa wa sensitivity ambavyo ndio hivi tunavyo
mitaani ambavyo kwa maabara huwa ni determining test tu. tunatolea majibu kama
majibu yakiwa negative tu lakini yakiwa positive tunatumia kipimo kingine
chenye specificity kuhakiki.
Kipimo hiki cha
kuhakiki (uni-gold) huwa hakitolewi kirahisi na hata ukitumia casset moja
lazima uitolee maelezo umeitumia kwa nani? na huyu mgonjwa lazima umpe refferal
aende CTC kupata ushauri nasaha na hata kuanza dawa. Sasa unaona ilivyo ngumu
kukipata sio.
Sasa yule dada akaenda
kujipima huko kwake kama kawaida mnaojipima mnaelewa mnafanya nini, wengine
wanaweka maji kwa kukosa maji maalumu ya kipimo (buffer) yule dada kupima
ikatokea mistari miwili, Acha yule dada achanganyikiwa hadi kuzimia.
Baada ya kuletwa
hospitali na kupatiwa huduma ya kwanza akazinduka ndipo akaeleza nini kimemkuta
ikabidi turudie kupima tena majibu yakaja negative. Kumbe huyu dada alikua na
maambukizi mengine ya kirusi lakini sio VVU.
Kwaiyo basi. Mashine za
maabara hutumiwa kwa kuzingatia asilimia za sensitivity na specificity.
0 Comments